RIPOTI RASMI YA MKUTANO MKUU WA CPT 2025
- CPT Media
- Nov 29, 2025
- 1 min read
Updated: Jan 12
Christian Professionals of Tanzania (CPT) ilifanya Mkutano wake Mkuu wa mwaka 2025 ukiwakutanisha wanataaluma Wakristo kutoka majimbo mbalimbali nchini kwa lengo la kutafakari, kujadili na kuweka mwelekeo wa utume wa CPT katika kulihudumia Kanisa na Taifa.
Mkutano huu uliweka msisitizo katika kuunganisha Imani, Taaluma na Jamii, kwa kuangazia masuala muhimu ya kijamii na kitaifa yakiwemo umoja wa kitaifa, haki, uchaguzi, maadili ya uongozi, ushiriki wa vijana na wanawake, pamoja na mwelekeo wa kimkakati wa CPT baada ya zaidi ya miaka 40 ya utume.
Ripoti hii imeunganisha mjadala na maazimio ya:
Siku ya Kwanza - Msingi wa kiroho, nafasi ya wanataaluma katika Kanisa na Taifa, tathmini ya hali ya kijamii na uchaguzi wa mwaka 2025, pamoja na vipaumbele vilivyoibuka.
Siku ya Pili - Tathmini ya safari ya CPT, ripoti za majimbo, changamoto za kiutendaji na kifedha, mabadiliko ya kidijitali, ushiriki wa vijana na wanawake, pamoja na maazimio ya kimkakati ya miaka ijayo.
Pakua Ripoti Kamili ya Mkutano Mkuu wa CPT 2025 hapa.




Comments