KUKANUSHA TAARIFA INAYOSAMBAA MITANDAONI
- CPT Media
- 5 days ago
- 1 min read
Uongozi wa CPT Taifa unapenda kutoa taarifa rasmi ya kukanusha taarifa yenye kichwa cha habari "TAARIFA RASMI YA CPT” (The Catholic Professionals of Tanzania) inayosambaa kwenye mitandao ya Kijamii hususani whatsapp, facebook nk.
Uongozi wa CPT unapenda kuwataarifu Viongozi, Wana CPT na Waumini wote mambo yafuatayo:
Taarifa hiyo iliyoandikwa na Dr. Nagaikaya Thomas M (PhD) sio taarifa rasmi ya Ofisi na wala mwandishi huyo sio Mwana CPT anayetambulika na hajapewa mamlaka yoyote ya kuandika taarifa kwa niaba ya CPT.
CPT chini ya Baraza la Maaskofu inao utaratibu wa kutafakari, kuchambua na kutekeleza mambo yake ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kadri ya mifumo, miongozo na taratibu za Kanisa na sio njia hiyo iliyotumika.
CPT inatambua haki ya kila mtu kujieleza na kutoa maoni yake. Hata hivyo, inalaani vikali utaratibu wa mtu yeyote kujivika mamlaka ya kutoa maoni yake kwa mwamvuli wa CPT. Kimsingi CPT haina desturi ya aina hii ya watu na hiki ni kiashiria tosha kwamba huyu sio mwenzetu.
Aidha, CPT inatambulika kama Christian Professionals of Tanzania na sio Catholic Professionals of Tanzania.
Kwa barua hii, tunawasihi wana CPT na wadau wote kupuuza ujumbe huo, na tunawaomba kutumia njia mwafaka katika kushirikisha mangamuzi yao na kutoa mchango wao wa kitaalamu kwa jamii kwa kuzingatia taratibu za CPT na Kanisa kwa ujumla.
Uongozi wa CPT unawatakia Utume mwema.
Katika Kristo,
Nakala rasmi ya barua yenye taarifa hii kutoka katika ofisi ya CPT taifa, imeambatanishwa pamoja na tangazo hili.





Comments