CPT Jimbo Kuu la DSM Wafanya Hija ya Kiroho Kuadhimisha Mwaka wa Jubilee 2025
Jumamosi, 05 Apr
|Kituo cha Kiroho cha Mbagala
Akinukuu maneno ya Baba Mtakatifu, "Matumaini hayatatutahayarisha, matumaini hayadanganyi" (Warumi 5:5), Padre Mavula aliwaalika wanataaluma kuingia katika hija ya kiroho; safari ya ndani ya mioyo yao ili kumfungulia Kristo nafasi ya kuingia, kuwataka na kuwaongoza katika maisha yao ya kila siku.


Time & Location
05 Apr 2025, 08:00 – 16:00
Kituo cha Kiroho cha Mbagala, Dar es Salaam, Tanzania
About the event
Katika shamrashamra za kuelekea Mwaka wa Jubilee 2025 , wanataaluma Wakristo (CPT) kutoka Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam walipata fursa adhimu ya kushiriki mafungo maalum ya kiroho. Mafungo haya yalifanyika Mbagala Spiritual Center na yalilenga kuwapatia wanataaluma hao nafasi ya kutafakari wajibu wao kama Wakristo katika jamii ya sasa, na jinsi wanavyoweza kuchangia katika ujenzi wa mapato, maadili na maendeleo ya kweli.
Mafungo haya yaliwezeshwa na Padre Dominick Mavula wa Shirika la Damu Azizi , ambaye pia ni Mkurugenzi wa Radio Maria Tanzania . Padre Mavula alitoa tafakari ya kina iliyojikita katika Ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko , kama ulivyoandikwa katika hati rasmi ya Jubilee. Akinukuu maneno ya Baba Mtakatifu, "Matumaini hayatatutahayarisha, matumaini hayadanganyi" (Warumi 5:5), Padre Mavula aliwaalika wanataaluma kuingia katika hija ya kiroho; safari ya ndani ya mioyo yao ili kumfungulia Kristo nafasi ya kuingia, kuwataka na kuwaongoza katika maisha yao ya kila siku.
Hija hii…
